Saturday 20/04/2024English (EN) | Swahili (SW)
Baraza la Vijana Zanzibar

HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA CHAKECHAKE

Baraza la vijana Wilaya ya Chake chake ni miongoni mwa mabaraza 11 ya Wilaya za Zanzibar, Baraza hili lilianzishwa tarehe 16/07/2016.Baraza la Vijana. Wilaya ya ChakeChake linajumuisha vijana kutoka shehia 32.

MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA WILAYA

  1. Mwenyekiti
  2. Makamo mwenyekiti
  3. Katibu /Afisa Vijana
  4. Pamoja na Wajumbe 7 wa kamati tendaji ambao wote wanachaguliwa kwa kupigiwa kura isipokuwa Katibu wa baraza la Vijana Wilaya ambae anakuwa afisa vijana Wilaya.

MALENGO YA BARAZA LA VIJANA CHAKECHAKE

  1. Kuwajenga Vijana kutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu na pia kuifahamu kwa kina jamii,kiuchumi,hali halisi kiutamaduni na upeo wake.
  2. Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar
  3. Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii;
  4. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA BARAZA lA VIJANA WILAYA YA CHAKECHAKE NI KAMA ZIFUATAZO:

  1. Kilimo cha mchai chai.
  2. Kilimo cha Mboga Mboga.
  3. Ushonaji
  4. Ufugaji wa ngo’mbe
  5. Ufugaji wa kuku
  6. Utengenezaji wa Sabuni za Maji.
  7. Mradi wa Usafi
  8. Kushiriki katika makongamao mbali mbali.
  9. Kushiriki katika mashindano mbali mbali ya michezo kama vile mpira wa miguu na basketball

MAFANIKIO KWA BARAZA LA VIJANA CHAKECHAKE

  1. Kutoa elimu kwa vijana na jamii kwa ujumla kupitia vyombo mbali mbali vya Habari, juu ya Madhara ya madwa ya kulevya, Mimba za umri mdogo, Udhalilishaji na Umuhimu wa vijana kufanya kazi za uzalishaji.
  2. Kushirikiana na Taasisi mbali mbali za kiserekali na zisizo za serikali kutoa elimu kwa vijana, elimu vijana kama vile elimu ya Afya ya uzazi, magonjwa ya ngono na Study za Maisha.
  3. Kuendeleza Shughuli za vijana kupitia miradi ya kiuchumi
  4. Kuanzisha darasa la Kundisha vijana mambo ya Utalii pamoja na Lugha za kigeni.
  5. Vijana kuwa wazalendo na kujitolea katika harakati mbali mbali za ujenzi wa Taifa.
  6. Kufungua kampuni ya usafi na kuweza kujiajiri wenyewe
Matangazo

Habari
Baraza la Vijana Taifa lafanya Kipidi na ZBC radio kinachoitwa Jukwaa la Vijana
play audio iliupate kusikiliza kipindi
Mitandao ya Kijamii

Facebook

Twitter

instagram

Utube

SLP:3501
Mwanakwerekwe
Zanzibar
SimuNamba:+2550655828181 | +255629222001
BaruaPepe:info@zyc.go.tz

Copyright © 2024. All right reserved. Baraza La Vijana Zanzibar.