Thursday 18/04/2024English (EN) | Swahili (SW)
Baraza la Vijana Zanzibar

HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR

Baraza la Vijana ni Chombo kinachojitegemea Kilichoanzishwa Chini ya Sheria namba 16 ya mwaka 2013 ambayo imetiwa saini tarehe 30/06/2014 na Mheshimiwa Rais Wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein

Baraza la Vijana la Zanzibar limeundwa kwa mujibu wa matakwa ya Kisera na Kisheria yanayoelekeza haja ya kuwajenga vijana kuutambua utaifa wao, hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu, pia kuifahamu kwa kina jamii, kiuchumi, hali halisi kiutamaduni na upeo wake; Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar; Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii na kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi.

Baraza hili limeundwa Baraza la Vijana Zanzibar limeundwa kwa Sheria Namba 16 ya mwaka 2013 ya Baraza la Vijana ambayo uundwaji wa Baraza hili umechangiwa na mambo muhimu yafuatayo:-

  1. Mkataba wa Haki za Binaadamu wa Afrika (Africa Youth Charter 1948)…………
  2. CEDAW………………………..
  3. Utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Zanzibar ya mwaka 2005, ambayo imelekezea juu ya uanzishwaji wa Baraza la Vijana na mwelekeo ya Kiresa unaotambua juu ya uwepo wa Baraza hili.
  4. Utekelezaji wa Makubaliano ya Mkataba wa Vijana wa Afrika (African Youth Charter - 2006) ambao umeridhiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania mwaka 2012. Mkataba huu unasisitiza nchi wanachama juu ya umuhimu wa kuwajengea uwezo vijana ikiwemo kuwa na chombo cha kuwashirikisha katika hatua mbali mbali za maendeleo katika jamii.
  5. Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 – 2015 iliyoelekezea umuhimu wa uundwaji wa Baraza la Vijana Zanzibar
  6. Utekelezaji wa Malengo Makuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (MKUZA) katika kuhakikisha vijana wanafikiwa na kuunganishwa katika fursa mbali mbali pamoja na kuwajegea mustakbali wa Kitaifa ili waweze kuwa na tamko la pamoja kwa masuala yanayowahusu ushiriki na ushirikishwaji wa vijana kwa maendeleo yao.

Aidha, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 – 2020 ibara 131(b) imeelezea pia juu ya uimarishaji na uendelezaji wa Baraza la Vijana ili kuongeza ushiriki wa vijana katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2010 – 2015 mwezi wa Aprili, 2015, Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alifanya uteuzi wa Katibu Mtendaji wa Baraza Zanzibar ambae ndiye Mtendaji na Mratibu wa Sekretarieti ya Baraza la Vijana Taifa kwa mujibu wa Sheria ya Kuanzisha Baraza la Vijana Zanzibar.

Baada ya uteuzi wa Katibu Mtendaji harakati na taratibu za uchaguzi kwa Mabaraza ya Vijana Kishehia, Wilaya na Kitaifa zikaanza. Mwezi Februari hadi Juni, 2016 ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa Mabaraza ya Vijana ngazi ya Shehia. Mwezi Juni hadi Julai 2016 ulifanyika uchaguzi wa viongozi ngazi za Wilaya na mwezi Septemba 2016 ulifanyika uchaguzi wa viongozi ngazi ya Taifa.

Viongozi waliochaguliwa ngazi za Shehia ni Wenyeviti, Makamo Wenyeviti, Katibu na wajumbe wa Kamati Tendaji za Shehia. Kwa ngazi za Wilaya viongozi waliochaguliwa ni Wenyeviti, Makamo Wenyeviti na Kamati Tendaji za Wilaya. Kwa ngazi za Wilaya Makatibu wa Mabaraza ya Vijana ni Maofisa Vijana wa Wilaya. Kwa ngazi ya Taifa viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti na Baraza la Watendaji Taifa. Kwa ngazi ya Taifa Sheria inatambua kuwepo kwa Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza akisaidiana na Wakuu wa Vitengo ambao ni waajiriwa wa Serikali.

MALENGO YA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR

  1. Kuwajenga Vijana kutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu na pia kuifahamu kwa kina jamii,kiuchumi,hali halisi kiutamaduni na upeo wake.
  2. Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar
  3. Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii;
  4. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi

KAZI ZA BARAZA LA VIJANA ZANZIBAR

  1. Kushauri na kushauriana na Wizara katika masuala yote ya vijana na mipango ya maendeleo
  2. Kushajihisha upatikanaji Wa haki za vijana Kupana wigo endelevu wa maendeleo ikijumuisha sera kanuni, sheria ,mambo ya kimsingi na mipango.
  3. Kuandaa ,kusimamia na kutathmini mipango ilioyoanzishwa na vijana ambayo yanaweza kupimwa baaddae na jumuiya za vijana sambamba na mipango ya Taifa.
  4. Kusaidia na kushajiisha vikundi vyenye maslahi na maendeleo ya vijana katika kuanzisha mafunzo kwa vijana na mipango ya maendeleo na utafiti ili kuunga mkono mipango iliyoshuhudiwa ya vijana na kukuza utumiaji wake.
  5. Kwa kushirikiana na Wizara Kuandaa nyaraka mbali mbali na kueneza taaluma iliyopatikana na mifano ya matendo ya kuigwa yanayohusiana na mipango ya vijana.
  6. Kuhamisisha na Kusambaza raslimali katika kuunga mkono utekelezaji wa mipango ya vijana na kuimarisha uwezo vikundi au jumuiya za vijana
  7. Kuanzisha ,kuendesha na kusimamia miradi yenye na isiyo letea faida katika kuunga mkono maendeleo ya Vijana kama itakavyoonekanwa inafaa
  8. Kupanga na Kuendesha mikutano ya Baraza la Vijana
  9. Kufanya kazi nyenginezo kama ambavyo Baraza litaona inafaa kufuatana na malengo yake.

Muundo wa Baraza La Vijana Zanzibar

  • Baraza la Vijana Taifa
  • Baraza vijana Wilaya
  • Baraza vijana Shehiya

Muundo wa Baraza La Vijana Shehiya

  • Mkutano Mkuu wa Shehia
  • Kamati Tendaji ya Shehia
SLP:3501
Mwanakwerekwe
Zanzibar
SimuNamba:+2550655828181 | +255629222001
BaruaPepe:info@zyc.go.tz

Copyright © 2024. All right reserved. Baraza La Vijana Zanzibar.