Wednesday 24/04/2024English (EN) | Swahili (SW)
Baraza la Vijana Zanzibar

HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA KUSINI

Baada ya Kupitishwa sheria namba 16 ya mwaka 2013 ya kuanzishwa Baraza la Vijana Zanzibar.Wilaya ya Kusini iliwashajihisha Vijana kujiunga na Baraza la Vijana Kupitia Shehia yao.

Baraza la Vijana Wilaya ya Kusini linajumuisha vijana kutoka shehia zote 21

MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA WILAYA

  1. Mwenyekiti
  2. Makamo mwenyekiti
  3. Katibu /Afisa Vijana
  4. Pamoja na Wajumbe 7 wa kamati tendaji ambao wote wanachaguliwa kwa kupigiwa kura isipokuwa Katibu wa baraza la Vijana Wilaya ambae anakuwa afisa vijana Wilaya.

MALENGO YA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA KUSINI

  1. Kuwajenga Vijana kutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu na pia kuifahamu kwa kina jamii,kiuchumi,hali halisi kiutamaduni na upeo wake.
  2. Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar
  3. Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii;
  4. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA KUSINI

  1. Kilimo cha mboga mboga
  2. Ujasiriamali
  3. Kilimo cha migomba
  4. Kilimo cha misitu
  5. Ufugaji nyuki
  6. Ufugaji kuku
  7. Ufugaji samaki
  8. Biashara

MAFANIKIO KWA BARAZA LA VIJANA KUSINI

  1. Baraza la Vijana ngazi ya Shehia wameweza kuendesha na kuendeleza miradi ya kilimo uvuvi na ufugaji.
  2. Vijana wamepata kujiajiri wenyewe bila kusubiri ajira serikalini
  3. Vijana wamepata kujua umuhimu wa uzalendo nchi yao.
  4. Vijana wamepata kujua elimu ya stadi za Maisha na kujiepusha na vikundi viovu
  5. Vijana wamepata kujua elimu ya Uongozi
Matangazo

Habari
Baraza la Vijana Taifa lafanya Kipidi na ZBC radio kinachoitwa Jukwaa la Vijana
play audio iliupate kusikiliza kipindi
Mitandao ya Kijamii

Facebook

Twitter

instagram

Utube

SLP:3501
Mwanakwerekwe
Zanzibar
SimuNamba:+2550655828181 | +255629222001
BaruaPepe:info@zyc.go.tz

Copyright © 2024. All right reserved. Baraza La Vijana Zanzibar.