Friday 19/04/2024English (EN) | Swahili (SW)
Baraza la Vijana Zanzibar

HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA MJINI

Baraza la Vijana Wilaya ya Mjini ni taasisi inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria nambari 16 ya mwaka 2013 ya uanzishwaji wa wa Baraza la Vijana Zanzibar. Baraza la Vijna Wilaya ya Mjini limeanza mnamo 18/07/2016.

MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA WILAYA

  1. Mkutano Mkuu Wilaya
  2. Kamati Tendaji Wilaya

MALENGO YA BARAZA LA VIJANA MJINI

  1. Kuwajenga Vijana kutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu na pia kuifahamu kwa kina jamii,kiuchumi,hali halisi kiutamaduni na upeo wake.
  2. Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar
  3. Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii;
  4. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA BARAZA lA VIJANA WILAYA YA MJINI NI KAMA ZIFUATAZO:

  1. Kutoa elimu ya Uongozi kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali
  2. Mradi Usafi wa mazingira
  3. Kutoa mafunzo ya habari na utangazaji kwa kushirikiana na taasisi ya Mwanza Youth and Children Network (MYCN)
  4. Kutoa elimu ya stadi za Maisha kwa Vijana
  5. Kilimo cha mboga mboga
  6. Ushonaji wa mashuka ya kudarizi
  7. Ufugaji wa kuku
  8. MAFANIKIO KWA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA MJINI

    1. Baraza la Vijana ngazi ya Shehia wameweza kuendesha na kuendeleza miradi ya kilimo na ufugaji.
    2. Vijana wamepata kujua umuhimu wa uzalendo nchi yao.
    3. Vijana wamepata kujua elimu ya stadi za Maisha na kujiepusha na vikundi viovu
    4. Vijana wameweza kupata ajira kupitia Baraza la Vijana
Matangazo

Habari
Baraza la Vijana Taifa lafanya Kipidi na ZBC radio kinachoitwa Jukwaa la Vijana
play audio iliupate kusikiliza kipindi
Mitandao ya Kijamii

Facebook

Twitter

instagram

Utube

SLP:3501
Mwanakwerekwe
Zanzibar
SimuNamba:+2550655828181 | +255629222001
BaruaPepe:info@zyc.go.tz

Copyright © 2024. All right reserved. Baraza La Vijana Zanzibar.