HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA KASKAZINI A
Baraza la Vijana Wilaya ya Kaskazini A ni taasisi inayojitegemea iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria nambari 16 ya mwaka 2013 ya uanzishwaji wa wa Baraza la Vijana Zanzibar. Baraza la Vijna Wilaya ya Mjini limeanza mnamo 18/07/2016.
MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA WILAYA
- Mkutano Mkuu Wilaya
- Kamati Tendaji Wilaya
MALENGO YA BARAZA LA VIJANA KASKAZINI A
- Kuwajenga Vijana kutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu na pia kuifahamu
kwa kina jamii,kiuchumi,hali halisi kiutamaduni na upeo wake.
- Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar
- Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii;
- Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi
SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA BARAZA lA VIJANA WILAYA YA KASKAZINI A NI KAMA ZIFUATAZO:
- Kutoa elimu ya Uongozi kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali
- Kutoa elimu ya kupambana na madawa ya kulevya.
- Kutoa elimu ya stadi za Maisha kwa Vijana
- Kilimo cha mboga mboga
- Ushonaji wa mashuka ya kudarizi
MAFANIKIO KWA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA KASKAZINI A
- Vijana wamepata elimu ya kupambana na Madawa ya kulevya
- Baraza la Vijana ngazi ya Shehia wameweza kuendesha na kuendeleza miradi ya kilimo na ufugaji.
- Vijana wamepata kujua umuhimu wa uzalendo nchi yao.
- Vijana wamepata kujua elimu ya stadi za Maisha na kujiepusha na vikundi viovu
- Vijana wameweza kupata ajira kupitia Baraza la Vijana