Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

Youth Future Hub

Utangulizi

Kwa kutambua kuwa changamoto na fursa zinazowakabili vijana hubadilika kwa kasi kubwa, Baraza la Vijana Zanzibar limeanzisha Programu ya Future Hub. Lengo kuu ni kuwajenga viongozi wa baadae wa Baraza la Vijana na pia kuwahamasisha vijana katika kutafuta fursa mbali mbali za kitaifa na kimataifa. Future Hub ni jukwaa la kuibua, kuimarisha na kuunganisha vijana ili wawe viongozi wa mabadiliko chanya katika shehia na ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Malengo ya Programu ya Future Hub
Kutoa Fursa za Ushiriki wa Mafunzo ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa
Kujenga Viongozi Bora wa Baadaye
Kuunganisha Vijana na Fursa za Kitaifa na Kimataifa
Kujenga Mtandao Imara wa Vijana
Kuhamasisha Maadili, Uwajibikaji na Uzalendo
Kuimarisha Baraza la Vijana
Taarifa za Miradi