Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

PROGRAM YA MOBILE YOUTH SPACE (MYS)

Baraza la Vijana Zanzibar ni taasisi ya Serikali iliopo chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ambayo imeanzishwa kupitia Sheria ya Baraza la Vijana Nam.16/2013 kwa lengo la kuwa Jukwaa na Kiungo wakilishi cha maslahi ya Vijana Zanzibar.

Katika utekelezaji wa shughuli zake kupitia Sheria hii, Baraza limeundwa na muundo wa ngazi ya Shehia, Wilaya na Taifa. Miongoni mwa malengo ya Baraza la Vijana Zanzibar ni kufanya kazi kama jukwaa na kiungo wakilishi kwa maslahi ya vijana Zanzibar katika kuhakikisha inakuza ushiriki na ushirikishwaji wa vijana pamoja na kuwajenga vijana kuutambua utaifa wao, hali ya umoja na mshikamano.

Kupitia malengo haya mawili, Baraza la Vijana limeandaa program mbili katika kuyafikia na kuleta ufanisi. Program ya mwanzo ni Mobile Youth Space (MYS) ambayo tutaitekeleza kwa pamoja na Shirika la SOS kwa lengo la kuimarisha ushiriki na upatikanaji wa taarifa kwa Vijana.

Vijana wengi bado wanakabiliwa na changamoto ya ushiriki na ushirikishwaji hususani katika mambo yanayowahusu na hatimaye kukosa fursa na nafasi mbali mbali katika jamii ikiwemo nafasi za maamuzi, uongozi, ajira na nyenginezo. Aidha, changamoto nyengine ni kukosa taarifa sahihi juu ya mambo mbali mbali yanayowahusu na yanayotokea katika jamii yetu, na changamoto kubwa zaidi ipo katika maeneo ya vijijini ukilinganisha na mjini.

Sera ya Maendeleo ya Vijana ya Zanzibar ya mwaka 2023 imeonesha wazi changamoto ya ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika ngazi za maamuzi, kupanga na kutekeleza mipango ya maendeleo ya Kitaifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa licha ya jitahada mbali mbali zinazochukuliwa.

Program hii ya MYS inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Aprili 2025 hadi Aprili 2028 na imebeba ujumbe wa:

“USHIRIKI, USHIRIKISHWAJI NA UPATIKANAJI WA TAARIFA SAHIHI KWA VIJANA NI MSINGI WA MAENDELEO ENDELEVU”

Lengo kuu la kauli mbiu hii ni kuhakikisha kuwa Vijana wa Zanzibar wanashiriki na kushirikishwa vilivyo katika mambo mbali ya jamii na nchi yao kwa ujumla ili kutekeleza kwa vitendo msingi mmoja wa Utawala Bora.

Ni matarajio yetu, kauli mbiu hii itakuwa ni chachu ya upatikanaji mazingira mazuri ya upatikanaji wa taarifa sahihi kwa vijana kwa lengo la kutimiza ndoto zao za kimaisha.

Ifahamike kuwa ushiriki wenye tija kwa vijana ni nguzo sahihi ya upatikanaji wa taarifa zinazowahusu na hatimaye kuleta tija iliokusudiwa. Hivyo, program hii ya MYS kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa Sekta ya Vijana itakuwa ni hatua kubwa ya kuwa na ushiriki na ushirikishwaji wa vijana hususani katika maeneo ambayo ni ngumu kufikika.

Program hii itatekelezwa kupitia mikutano mbali mbali ya wazi (Public Meetings) kwa vijana katika Wilaya zote za Unguja na Pemba kwa kuwafata vijana katika maeneo yao. Inatarajiwa kufikiwa Vijana 39,600. Aidha, itajumuisha shughuli mbali mbali ikiwemo:

Katika mikutano itakayofanyika, kila mkutano wa vijana utajumuisha mada mbili pamoja na majadiliano juu ya mada husika ambazo zinawahusu vijana.

Taarifa za Miradi