Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

KAMPENI YA “IMARISHA MABARAZA YA VIJANA ZANZIBAR”

Utangulizi

Kampeni ya Imarisha Mabaraza ya Vijana Zanzibar ni kampeni ya kuyasimamisha na kuyaimarisha Mabaraza ya Vijana Zanzibar kiutendaji. Kampeni hii imekuja baada ya Baraza la Vijana Zanzibar kupitia shughuli zake za kila siku kufanya ziara kwa Mabaraza ya Vijana Wilaya zote za Unguja na Pemba kuanzia 15 Oktoba 2024 hadi 06 Novemba 2024. Lengo lilikuwa kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo pamoja na hadhi ya Mabaraza ya Vijana kwa ngazi zote za Wilaya na Shehia, sambamba na utambulisho wa Katibu Mtendaji mpya wa Baraza alieteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar tarehe 25 Septemba 2024.

Baadhi ya changamoto zilizobainika ni:

Hivyo, kuleta uhai kwa Mabaraza ya Vijana ni hatua muhimu ya kuhakikisha kuwa sauti za Vijana zinawasilishwa, changamoto zao zinapewa kipaumbele, na mchango wao katika maendeleo unatambuliwa.

Kampeni hii ilizinduliwa rasmi na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, ndugu Fatma Hamad Rajab tarehe 30 Novemba 2024 katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Tumekuja.

Lengo Kuu
Muda wa Kampeni

Kampeni hii ni ya miaka mitatu (3), kuanzia 1 Januari 2025 hadi 31 Disemba 2027.

Malengo Mahsusi
Mikakati ya Kampeni
Matokeo Yanayotarajiwa
Hitimisho

Ni wakati sahihi sasa kuleta uhai wa Mabaraza ya Vijana Zanzibar ili kutimiza adhma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba Baraza la Vijana ni jukwaa na kiungo wakilishi cha maslahi ya Vijana. Hivyo, Baraza litafanya mashirikiano na wadau mbali mbali ili kufanikisha malengo hayo. Kampeni hii itakuwa kiungo muhimu cha Mabaraza ya Vijana kwa ngazi ya Shehia, Wilaya na Taifa.

Taarifa za Miradi