Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

Mawasiliano - Baraza la Vijana Zanzibar

Waziri waVijan, Ajira na Uwezeshaji awataka Vijana wa Mabaraza ya Vijana Kuchagua Viongozi Bora.

News Image

Mwandishi: Bahati Habibu Peter

Tarehe: Monday, 19th January 2026

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe Shaaban Ali Othman ameyataka Mabaraza ya Vijana kufanya Uchaguzi na kuchagua viongozi watakaofaa kuongoza mabaraza hayo na kuwa sauti kwa vijana wengine ili kupata vijana wenye maono na wenye kuleta tija kwa Taifa.

Ameyasema hayo katika Skuli ya Berru foundation kwa Mtumwa Jeni Wilaya ya Mjini wakati akizungumza na Vijana wa Wilaya hiyo ikiwa ni ziara yake ya kutembelea vijana katika Shehia na kuzungumza nao ikiwa ni pamoja na kuzitolea ufafanuzi wa changamoto za Vijana

Amesema kuwa wapo vijana ambao wana maono mazuri na kuweza kuyafikisha mbali mabaraza hayo kwamaslahi yao Vijana kwa kuwa sauti ya Vijana

Akizungumzia kuhusu ajira amesema kuwa atahakikisha ajira zote ambazo anazisimamia zinaanzia katika ngazi ya Shehia sambamba na fursa masomo na mafunzo ya ndani na nje ya nchi

Amefahamisha kuwa atahakikisha kuwa ajira hizo ni bure na endapo atajitokeza mtu kuchukua pesa kwa lengo la kutoa ajira atachukuliwa hatua za kisheria.

" Jukumu letu sisi kama Viongozi ni kuhakikisha tunazisimamia fursa za Vijana ili vijana waweze kuzipata na kuzitumia fursa hizo na kufaidika nazo"alifafanua waziri

Mhe Shaaban amemtaka Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana kuandaa miradi mbalimbali itakayoendana na vijana ili kuwainua kiuchumi

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhe, Salama Mbaruok Khatib ameeleza kuwa uwepo wa Mabaraza ya Vijana ni moja ya kufanikisha adhma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuanzishwa kwa Baraza la Vijana Zanzibar na kuwataka vijana kuitumia ipasavyo fursa hiyo

Amefahamisha kuwa viongozi Wakuu wa Serikali wamekua na mtazamo chanya kwa vijana ili kufahamu na kutatua changamoto za Vijana hivyo kila Kijana atambue fursa atajayoipata kwa kujiunga na Baraza

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi wa mabaraza ya vijana Katibu Salama amesema kuwa wakati umefika kuhakikisha vijana wanafanya Uchaguzi na kuwataka masheha kuwahamasisha vijana kugombea nafasi za Uongozi ili kuwa na mabaraza yaliohai kwa utendaji kazi

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Vijana Ali Haji Hassan amesema kuwa msingi wa mabaraza ya vijana ni Shehia hivyo ni vyema kuhamasisha vijana ili kujiunga katika mabaraza hayo na kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi

Aidha amesema kuwa msingi mkuu wa Serikali kuhakikisha vijana sauti zao zinasikika hivyo ameahidi kuendelea kuhamasisha vijana kuthamini na kuunga mkono mabaraza hayo kwa kutoa changamoto zao ili kutafutiwa ufumbuzi

Nao vijana wa Wilaya hiyo kutoka Shehia mbalimbali wameomba kusaidiwa kupitia mabaraza hayo sambamba na kupatiwa mitaji au mikopo itakayowasaidia kujikwamua kiuchumi na kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Aidha wameomba kupatiwa vifaa visaidizi kwa watu Wenye mahitaji maalum ili kurahisisha kazi zao sambamba na kupewa mitaji au kuanzishiwa miradi itakayowafanya wajiajiri badala ya kukaa na kusibiria ajira kutoka Serikalini kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza wimbi la Vijana kusubiri Ajira

Taarifa za Miradi