Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

Mawasiliano - Baraza la Vijana Zanzibar

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe, Shaaban Ali Othman amewataka vijana kuchagua viongozi wenye uwezo na sifa ya kuwasimamia Vijana wenzao kuanzia ngazi ya Shehia .

News Image

Mwandishi: Bahati Habibu Peter

Tarehe: Saturday, 24th January 2026

Waziri wa Vijana, Ajira na Uwezeshaji Mhe, Shaaban Ali Othman amewataka vijana kuchagua viongozi wenye uwezo na sifa ya kuwasimamia Vijana wenzao kuanzia ngazi ya Shehia .

Ameyasema hayo katika muendelezo wa ziara ya kuzungumza na Vijana huko Uwanja wa Granada Welezo Wilaya ya Magharibi 'A'

Amesema uchaguzi utakaofanyika uwe wa huru na haki sambamba na uadilifu katika kuchagua viongozi ambao watakuwa ni sauti ya kuwasemea changamoto zao sambamba na kuimarisha uhai Mabaraza ya Vijana Katika ngazi ya Shehia Wilaya hadi Taifa

Aidha amesema Wizara hiyo imejipanga kuzalisha Ajira mbali mbali ikiwemo ajira za Serikali Sekta binafsi,pamoja na kupatiwa fedha za kujiendeleza katika kuimarisha mitaji ya Biashara zao

Amewataka Vijana kutokubali kutoa rushwa katika Masuala ya ajira kwani Serikali wala sekta binafsi haitoi ajira kwa fedha hivyo kutoa rushwa ni kosa kisheria .

Ameeleza kwamba Wizara itahakikisha inazalisha Ajira na kuwaletea Vijana ili kuendelea kuwa raia wema katika nchi yao na kuona Ustawi wao unaimarika.

Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Vijana Ali Haji Hassan amewataka Vijana waendelee kuwahamasisha Vijana wenzao ili waweze kuitumia fursa ya kuchagua na kuchaguliwa katika Uchaguzi wa Mabaraza ya Vijana .

Kwa Upande wa Kamishna wa Kinga Tiba na Marekebisho ya Tabia kutoka Mamlaka ya dawa za kulevya Juma Abraham Zidikheir amesema waathirika wakubwa wa madawa ya kulevya ni Vijana ambao hupata matatizo ya afya ya akili .

Ameeleza kuwa baadhi ya Watumiaji wa uraibu hupoteza ajira,afya ya mwili sambamba na kuathiri familia zao kupata vifungo vya muda mrefu pamoja na kutaifishwa mali zao.

Taarifa za Miradi