Email:info@zyc.go.tz
   

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

Baraza la Vijana Zanzibar

Mawasiliano - Baraza la Vijana Zanzibar

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Moh’d Abrahman Juma, leo ameshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha Inua Vijana na TEHAMA kilichopo Mwanakwerekwe, Zanzibar

News Image

Mwandishi: Afisa Habari

Tarehe: Thursday, 9th April 2026

Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Zanzibar, Moh’d Abrahman Juma, leo ameshiriki katika hafla ya uzinduzi wa kituo cha Inua Vijana na TEHAMA kilichopo Mwanakwerekwe, Zanzibar ikiwa ni miongoni mwa miradi inayozinduliwa kwa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026.

Hafla hiyo imehudhuriwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana, viongozi wa jamii pamoja na vijana wenyewe waliokuja kushuhudia hatua hiyo muhimu inayolenga kuwawezesha vijana katika nyanja ya teknolojia na ubunifu.


Kituo hicho kimefadhiliwa na Shirika la SOS Zanzibar kwa lengo la kukuza ujuzi wa kidijitali miongoni mwa vijana na kuwasaidia kujiajiri au kupata ajira kupitia sekta ya TEHAMA


Akizungumza katika uzinduzi huo, Moh’d Abrahman Juma ameishukuru SOS Zanzibar kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya vijana, akisisitiza kuwa uwekezaji katika maarifa na teknolojia ni njia sahihi ya kuijenga Zanzibar yenye ushindani wa kiuchumi.
Aidha, kituo hicho kinasimamiwa na Baraza la Vijana Zanzibar, ambapo kitatoa mafunzo mbalimbali ikiwemo matumizi ya kompyuta, ubunifu wa kidijitali na ujasiriamali wa kisasa

Uzinduzi wa kituo hiki unatarajiwa kuwa chachu ya mabadiliko kwa vijana wa Mwanakwerekwe na maeneo jirani, kwa kuwapatia fursa mpya za kujifunza na kujiendeleza katika dunia ya sasa inayotegemea teknolojia.

Taarifa za Miradi