Friday 26/04/2024English (EN) | Swahili (SW)
Baraza la Vijana Zanzibar

HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA MAGHARIBI "A"

Baada ya Kupitishwa sheria namba 16 ya mwaka 2013 ya kuanzishwa Baraza la Vijana Zanzibar.Wilaya ya Magharibi “A” iliwashajihisha Vijana kujiunga na Baraza la Vijana Kupitia Shehia yao.

Harakati za uhamasishaji wa uanzishwaji wa mabaraza ya Vijana ulifanyika kwa Shehia zote 31 za Wilaya ya Magharibi “A” kwa mashirikiano ya vijana wa kujitolea .Viongozi wa Wilaya pamoja na masheha wa Shehia husika, ikiwa hadi sasa zoezi hilo linaendelea kufanyika.

Zoezi la Utoaji wa fomu za uwanachama za kujiunga na Baraza la Vijana kwa hiari lilifanyika kwa hatua ambayo iliwezesha kufanyika kwa uchaguzi kuanzia ngazi ya Shehia hadi Wilaya.

MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA WILAYA

  1. Mkutano Mkuu Wilaya
  2. Kamati Tendaji Wilaya

MALENGO YA BARAZA LA VIJANA MAGHARIBI "A"

  1. Kuwajenga Vijana kutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano na kujiheshimu na pia kuifahamu kwa kina jamii,kiuchumi,hali halisi kiutamaduni na upeo wake.
  2. Kufanya kazi kama ni jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Zanzibar
  3. Kushajiisha kujengewa uwezo vijana ili kuwafanya wazalishaji katika jamii;
  4. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA BARAZA lA VIJANA WILAYA YA MAGHARIBI “A” NI KAMA ZIFUATAZO:

  1. Kutoa mafunzo mbali mbali ya stadi za Maisha na Ujasiriamali kwa vijana
  2. Kutoa mafunzo ya uongozi
  3. Kufanya usafi katika Shehia
  4. Kilimo na ufugaji wa kuku
  5. Utengezaji wa viti na meza kwa kutumia maringi ya gari na dastubini za chupa
  6. Ushonaji wa nguo na kudarizi mashuka
  7. Kutoa elimu ya uzalendo kwa vijana

MAFANIKIO

  1. Baraza la Vijana ngazi ya Shehia wameweza kuendesha na kuendeleza miradi ya kilimo uvuvi na ufugaji.
  2. Vijana wamepata kujua umuhimu wa uzalendo nchi yao.
  3. Vijana wamepata kujua elimu ya stadi za Maisha na kujiepusha na vikundi viovu
  4. Vijana wamepata kujua elimu ya stadi za maisha
Matangazo

Habari
Baraza la Vijana Taifa lafanya Kipidi na ZBC radio kinachoitwa Jukwaa la Vijana
play audio iliupate kusikiliza kipindi
Mitandao ya Kijamii

Facebook

Twitter

instagram

Utube

SLP:3501
Mwanakwerekwe
Zanzibar
SimuNamba:+2550655828181 | +255629222001
BaruaPepe:info@zyc.go.tz

Copyright © 2024. All right reserved. Baraza La Vijana Zanzibar.