Friday 26/04/2024English (EN) | Swahili (SW)
Baraza la Vijana Zanzibar

HISTORIA YA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA MAGHARIBI B

Baraza la Vijana Wilaya ya Magharibi B ni Taasisi ilioanzishwa mwaka 2016 chini ya sharia no.16 ya mwaka 2013 ya uanzishwaji wa mabaraza ya vijana Zanzibar.Baraza la Vijana wilaya Magharibi “B” lilianza rasmin mnamo mwezi wa tisa mara tu baada ya kupata uongozi chini ya mlezi wao mkuu wa wilaya ya magharibi B.

MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA WILAYA MAGHARIBI "B"

  1. Mwenyekiti
  2. Makamo mwenyekiti
  3. Katibu /Afisa Vijana
  4. Pamoja na Wajumbe 7 wa kamati tendaji ambao wote wanachaguliwa kwa kupigiwa kura isipokuwa Katibu wa baraza la Vijana Wilaya ambae anakuwa afisa vijana Wilaya.

MALENGO YA BARAZA LA VIJANA MAGHARIBI "B"

  1. Kufanya vikao vya baraza la Vijana kwa lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu yao.
  2. Kuwashajihisha vijana kujiunga katika mabaraza ya vijana ndani ya shehia sambamba na kutoa fomu kwa vijana wanaotaka kujiunga na mabaraza
  3. Kuimarisha na kuendeleza vijana kwa kuwaunganisha na shughuli zote za kisiasa,kiuchumi na kijamii
  4. Kutembelea vikundi vya vijana kwa lengo la kuona utekelezaji wao na kutatua changamoto zinazowakabili
  5. Kuwashajiisha vijana waliokuwepo ndani ya mabaraza kuanzisha mifuko ya kuweka na kukopa (saccoss) kwa lengo la kujikwamua na Maisha.
  6. Kufanya shughuli mbali mbali kwa ajili ya kuadhimisha siku ya vijana duniani.

SHUGHULI ZINAZOFANYWA NA BARAZA lA VIJANA WILAYA YA MAGHARIBI "B" NI KAMA ZIFUATAZO:

  1. Kutoa elimu ya Uongozi kwa kushirikiana na taasisi mbali mbali
  2. Mradi Usafi wa mazingira
  3. Kutoa elimu ya stadi za Maisha kwa Vijana
  4. Kilimo cha mboga mboga
  5. Ushonaji wa mashuka ya kudarizi
  6. Ufugaji wa kuku
  7. Ujasiriamali kama vile utengezaji wa sabuni za mkaratusi,mwani,mafuta,shampoo,Arrow
  8. MAFANIKIO KWA BARAZA LA VIJANA WILAYA YA MAGHARIBI "B"

    1. Kuweza kuwaunganisha pamoja vijana waliomo ndani ya wilaya ya magharibi B
    2. Kujenga mahusiano na mashirikiano na mashirika na taasisi mbali mbali za kiserikali na watu binafsi nje na ndani ya nchi
    3. Kuwa ni chombo pekee kinachowasomea vijana na kutafuta njia ya kutatua changamoto zao ndani ya wilaya ya magharib “B”
Matangazo

Habari
Baraza la Vijana Taifa lafanya Kipidi na ZBC radio kinachoitwa Jukwaa la Vijana
play audio iliupate kusikiliza kipindi
Mitandao ya Kijamii

Facebook

Twitter

instagram

Utube

SLP:3501
Mwanakwerekwe
Zanzibar
SimuNamba:+2550655828181 | +255629222001
BaruaPepe:info@zyc.go.tz

Copyright © 2024. All right reserved. Baraza La Vijana Zanzibar.